Jumatano 1 Oktoba 2025 - 07:14
Ujumbe wa Hawza kutoka Qom Iran Watembelea Nyumba za Mashahidi  wa Hizbullah

Hawza / Ujumbe wa Hawza wa Jamhuri ya Kiislamu Iran, ukiwa katika miji ya Lebanon, ulizitembelea na kuziheshimu familia za mashahidi watatu wa Hizbullah.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Husayni Kuhsari, katika mazungumzo yake na Shirika la Habari la Hawza nchini Lebanon, alisema: ujumbe wa Hawza, uliosafiri Lebanon kwa ajili ya kushiriki katika kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa shahada ya Sayyid Hassan Nasrallah, ulifanya safari kutoka Beirut kuelekea miji ya kusini mwa Lebanon, ambapo katika miji miwili ya Nabatieh na Jibshit walishiriki katika shughuli mbalimbali, ikiwemo kuwatembelea mashahidi watatu wa kiroho wa Hizbullah Lebanon.

Akaongeza kuws: katika mpango huu, kwa kuzitembelea familia za mashahidi watatu wa kiroho wa Muqawama Hizbullah, waliheshimu daraja tukufu la mashahidi hao na kuwasilisha ujumbe wa wanahawza, wanazuoni na maulamaa wa Qom na Iran kwa familia hizo tukufu. Katika ziara hiyo waliheshimika mashahidi watatu: Shaykh ‘Ali Aburiyya, Shaykh ‘Abduh na Shaykh Sayyid al-‘Amili.

Naibu wa masuala ya kimataifa wa Hawza alibainisha: jambo la kuvutia katika ziara hizo tatu ni kwamba familia za mashahidi, huku zikishukuru Hawza kwa kuzitembelea nyumba za mashahidi hak, zililiona jambo hilo kuwa ni lenye thamani kubwa na la kuwatia moyo. Katika moja ya ziara hizo, mtoto mmoja wa shahidi alisema: “Baada ya shahada ya baba tulijihisi yatima, kwani shahada ya baba yetu ilitokea baada ya shahada ya Sayyid Hassan Nasrallah. Lakini leo, kwa uwepo wa wanazuoni na wanahawza ya Qom, hisia ya uyatima imeondoka, kana kwamba baba zetu wa kimaana wamekuja na kututoa kwenye hali ya yatima.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha